BALOZI DKT. NCHIMBI ATOA WITO KWA WAHITIMU WA CHUO KIKUU MZUMBE KUCHANGIA NA KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO YA CHUO

Mgeni maalum katika Mkutano wa 24 wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewahamasisha wahitimu kuchangia maendeleo ya taifa na kusaidia miradi ya maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe ili kuchochea maendeleo endelevu.

Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayo leo Novemba 23, 2024 katika mkutano muhimu wa 24 wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe uliohudhuriwa na wahitimu wa zamani (alumni), viongozi wa Chuo, na wadau mbalimbali wa elimu.

“Chuo Kikuu Mzumbe kimewapa msingi wa mafanikio yenu. Ni jukumu lenu kuhakikisha mnarudisha shukrani kwa kuchangia maendeleo ya Chuo ili kuwasaidia wengine kupata fursa kama zenu,” amesema Balozi Nchimbi.

Rais wa Baraza la Wahitimu, CAG Mstaafu CPA. Ludovick Utouh, amewahimiza wahitimu kuendelea kuwa mabalozi wa Chuo katika jamii zao kwa kudhihirisha weledi walioupata kutoka Chuo Kikuu Mzumbe.

Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amewahimiza wahitimu kuendelea kushirikiana na Chuo ili kuimarisha programu za masomo na kuboresha miundombinu.

“Baraza hili ni fursa ya kuimarisha uhusiano kati ya Chuo na wahitimu wake, ambao ni mabalozi wetu katika jamii. Tunategemea mchango wenu katika kufanikisha malengo yetu ya maendeleo endelevu,” alisema Prof. Mwegoha.

Kwa upande wake, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma), Prof. Eliza Mwakasangula, amesisitiza umuhimu wa wahitimu kuwekeza katika utafiti na uvumbuzi ili kushughulikia changamoto za kijamii.

“Umahiri wa wahitimu wetu ni urithi tunaoujivunia. Tunaamini katika uwezo wenu wa kuleta mabadiliko makubwa kupitia maarifa na ujuzi mliopata.”Alisisitiza Prof. Mwakasangula.

Mkutano huo umezaa matunda ya kipekee, ambapo wahitimu walijitolea kuunga mkono kupitia michango ya pesa taslimu na ahadi, huku baadhi yao wakikubali kushirikiana na Chuo katika shughuli za kujenga mazingira bora ya elimu. Hii ni ishara ya namna ambavyo wahitimu wanaweza kuchangia maendeleo ya Chuo na taifa kwa ujumla

********************

*****

 

*****

******

****

*****

 

*****

******

 

 

Contact Us

Vice Chancellor,

Mzumbe University,

P.O.BOX 1,

Mzumbe, Morogoro.


Tel: +255 023 2604380/1/3/4
Fax: +255 023 2931216
Cell: +255 0754 694029
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.